Yesu aliwaita wanafunzi wake ili awazoeze na kuwafunza ili baadaye awatume ulimwenguni kutangaza mambo yale waliyoyaona na kusikia kwake. Madaraka waliyopewa yalikuwa muhimu sana ambayo watu hawajapewa kama hayo. Madaraka yao yalikuwa ya pili kwa yale ya Kristo mwenyewe. Kazi yao ilikuwa kushirikiana na Mungu ili kuuokoa ulimwengu.Tumaini la Vizazi Vyote 158.4
Kuhusu Idara ya Huduma Za Kichungaji na Familia
Wachungaji ni watu wenye shughuli nyingi. Wanafanya kazi nyingi muhimu sana kuhudumia jamii zetu. Idara ya Huduma za Kichungaji husaidia kuandaa wachungaji, familia zao na viongozi wao wa mitaa na makanisa na kuwasaidia katika kuhudumia mahitaji ya makutaniko yao na kwa kuwa waadventista wa sabato ni waumini wakubwa wa maisha ya familia yenye furaha, Idara hii pia imejumuishwa na huduma za familia. Hii hulifanya kanisa kuimarisha familia kupitia huduma kama vile miongozo kabla ya ndoa, semina za ndoa, mafunzo kwa wazazi, na elimu maalum ya Biblia inayolenga familia.

Pr. NDIGANI A. NGONDO
MKURUGENZI WA HUDUMA – LTF